KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 22, 2014

BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA TANZANIA IMEANZISHA MASOMO YA JIONI YA DIPLOMA YA UKUTUBI

1
 Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Bw. Comfort Komba (kushoto), akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za Wilaya za Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bi. Georgina Misama.

Na Mwandishi wetu
  Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015.
  Hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo baada ya kuhitimu mafunzo ya cheti.
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Bw. Comfort Komba, wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Comfort alisema kuwa, masomo hayo kwa awali yalikuwa yakitolewa katika kampasi ya Bagamoyo lakini kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa masomo hayo ambapo mpaka sasa kuna wanafunzi wapya 130.
  “Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, imeamua kuanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015 na utaratibu huu tunautekeleza kutokana na kuwepo kwa ongezeko la uhitaji wa wanafunzi” Alisema Comfort.
  Aidha Comfort alisema kuwa, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kwa kushirikiana na halmashauri za Wilaya na Mikoa, imefanikiwa kuanzisha maktaba katika Wilaya mbalimbali ikiwemo Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu.
  Akizungumzia kuhusu uhifadhi wa machapisho ya kitaifa, Comfort alisema kuwa, Ofisi hiyo imefanikiwa kuhifadhi jumla ya vitabu 1,300,000 pamoja na majarida 950,000 tangu Bodi hiyo ilipoanzishwa katika ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi Tarafa.
  Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ni Shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

No comments:

Post a Comment