KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 24, 2014

CHIKAWE AIBOMOA NGOME YA CHADEMA NACHINGWEA

PIX 1..
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akimkabidhi kadi ya CCM, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilayani humo, Manufreda Mathias Malenga. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chama chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi, aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani Wilayani humo.
PIX 2.. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akimpongeza Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Kata ya Mtua, Habibu Oswadi (kushoto), baada ya kukabidhi kadi ya chama chake.
PIX 3.. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya, Kata pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja uliopo jirani na Ofisi za CCM Kata ya Mtua katika sherehe kubwa ya kuwapokea viongozi wawili na wanachama 21 wa Chadema waliojiunga na CCM Wilayani humo.   Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi, ambapo aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo.
PIX 4.. 
Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Nachingwea, Manufreda Mathias Malenga akizungumza kwa hisia baada ya kupewa nafasi kueleza furaha yake baada ya kukabidhi kadi ya Chadema na kupewa kadi pamoja na sare za CCM. Malenga aliwashukuru Viongozi na wanachama wa CCM kwa kumkaribisha katika chama hicho na kuahidi kutoa ushirikiano wake ndani ya chama hicho. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chama chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati meza kuu), alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo.
PIX5.. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (watano kulia waliosimama), akiwa na wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukikimbia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Wananchama hao 23 wakiongozwa na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa chama hicho Wilayani Nachingwea, Manufreda Malenga (watano kushoto waliosimama), walifanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo.

No comments:

Post a Comment