KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 21, 2014

DIAMOND MATATANI KWA KUVAA SARE ZA JESHI

 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kuwa limewasiliana na Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua za kisheria dhidi ya msanii Nassib Abdul 'Diamond Platinumz', kutokana na kuvaa nguo za kijeshi akiwa jukwaani.
Diamond katika Tamasha la Fiesta, lililofanyika juzi katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam, akiwa na madansa wake takribani wanne, walivaa sare za jeshi katika shoo yao.
Waliimba na kucheza takribani dakika 30, nyimbo za Diamond na kisha kuungana tena na msanii Ney wa Mitego, kuimba wimbo wao wa Mziki Gani, ambapo Ney naye alikuwa amevalia nguo za jeshi.

Diamond alirejea tena jukwaani kuimba na msanii mwingine kutoka Nigeria, Adedeji Adeleke 'Davido', kuimba wimb wao wa 'My Number One, remix'.
dmn 
Diamond na Davido, wakiwa jukwaani wakitumbuiza, Fiesta 2014.

No comments:

Post a Comment