KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 22, 2014

UNESCO YAFADHILI MAENDELEO YA SAYANSI AFRIKA

IMG_7570Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini Arusha
IMG_7483Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
IMG_7487Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
IMG_7359
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
IMG_7492Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)                                              

Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha.
Alisema shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.
“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema Naibu Mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment