BAADHI ya wabunge waliochangia hoja ya dharura bungeni leo wamewataka
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe, wawajibishwe.
Hayo yametolewa wakati wa kujadili Hoja ya Dharura kuhusu kupigwa kwa
baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo mwenyekiti wake,
Prof. Ibrahim Lipumba na baadhi ya wanachama wake juzi huko
Mtoni-Mtongani jijini Dar es Salaam.
SPIKA MAKINDA: Spika wa Bunge, Anne Makinda, alianza kwa kusema kuwa
wabunge wachangie hoja hiyo kwa dakika tatu.WAZIRI CHIKAWE: Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alianza kwa kusoma ripoti ya
serikali kuhusu kilichotokea wakati wa mkusanyiko wa wanachama wa CUF.
Alisema jeshi la polisi lilipokea taarifa kuhusu nia ya chama hicho
kufanya maandamano na mkutano wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa
Januari 27, 2001 huko Zanzibar.
Aliongeza kwamba kutokana na masuala ya kiusalama jeshi la polisi
liliona si vyema kuruhusu maandamano hayo lakini wafuasi wa chama hicho
waliamua kukiuka amri hiyo na kukusanyika huko Mbagala Januari 27, mwaka
huu ambapo walidhibitiwa na polisi.
MWANASHERIA MKUU: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju,
aliomba hoja ya dharura kuhusu polisi kuwapiga viongozi na wanachama wa
CUF juzi isijadiliwe bungeni maana suala lipo mahakamani.
TUNDU LISSU: Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alianza kwa
kukataa wabunge kuchangia mada kwa dakika tatu, akisema Waziri Chikawe
alikuwa amepewa dakika 30, na Mwanasheria Mkuu akipewa dakika 15.
Asema sheria inamruhusu mbunge kuchangia dakika zisizozidi dakika 15
hivyo Lissu alisema angetumia dakika 15 ila Spika aliingilia kati na
kusema wangetumia dakika 10 na Lissu akakubali.Lissu alisema mrithi wa
Werema (Mwanasheria Mkuu wa sasa, Mh. Masaju) si mshauri wa bunge
akiongeza kwamba bunge likitaka ushauri litamfuata Katibu wa Bunge.
Aliongeza kuwa ‘waziri wa mapolisi’ (Chikawe) ameongea uongo na
kudhihirisha kuwa kauli ya 'Wapigwe Tu' (iliyowahi kutolewa na Waziri
Mkuu Pinda bungeni) si ya bahati mbaya.Alisema viongozi wa upinzani
wanapigwa kwa kuwa kuna mafasisti serikalini na katika jeshi la polisi
akiongeza kwamba kazi ya polisi si kukataza maandamano bali ni
kuyaratibu.
Alilijulisha bunge kuwa hivi sasa wapinzani wana kesi nyingi
walizofunguliwa na polisi kwa njama wanazozijua na amelitaka bunge
kuchukua hatua na kuwawajibisha Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi kwa tukio hilo la juzi.
MHE. HABIB MNYAA: Mbunge wa CUF Mkanyageni, Habib Mnyaa, alisema
ombi la kufanya maandamano lilipelekwa tangu Januari 22 na si 27 kama
alivyosema Mh. Chikawe, mwaka huu na maandalizi yakafanyika ila jambo la
kushangaza ni kwamba taarifa kutoka jeshi la polisi kusitisha
maandamano hayo ilitolewa siku yenyewe ya maandamano asubuhi ya Januari
27, 2015.
Alihoji kwa nini nguvu zinazotumiwa na jeshi hilo kuwapiga wanachama
wa CUF zisitumike kupambana na majambazi wanaovamia vituo kama kule
Ikwiriri na Tanga?Katika kuhitimisha, alitaka jeshi la polisi livunjwe
na Waziri Mkuu ajiuzulu.
MBOWE: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,
alisema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Waziri Chikawe bungeni
kwani alivyoongea na baadhi ya maofisa wa polisi makao makuu walimwambia
agizo la kupigwa wafuasi wa CUF lilitoka ngazi za juu.
Akisisitiza alisema yeye na wenzake wamewahi kushambuliwa mara nyingi
na jeshi hilo lakini pamoja na kuripoti kwenye vyombo husika mpaka sasa
hakuna ufutialiaji wowote uliofanyika.
Asema baadhi ya wabunge wanacheka bungeni maana hawajawahi kujeruhiwa na polisi na wanaouawa na kupigwa na polisi si ndugu zao.
Asema baadhi ya wabunge wanacheka bungeni maana hawajawahi kujeruhiwa na polisi na wanaouawa na kupigwa na polisi si ndugu zao.
MBATIA: Mbunge James Mbatia alisema uamuzi uliofanywa na serikali
kuikimbizia mahakamani kesi dhidi ya Prof. Lipumba si sahii kwani
zilikuwa ni njama za kutaka suala hilo lisijadiliwe bungeni.Hata hivyo,
alimshukuru Spika wa Bunge kuruhusu mjadala ufanyike bungeni ambapo
alisema ukweli utaliweka taifa letu huru, kwani mtu yeyote anayemwaga
damu ya mwenzake ni gaidi na hawezi kuvumiliwa.
Mbatia aliongeza kuwa vitendo hivyo vilivyofanywa na polisi vinajenga
uhasama ndani ya taifa letu na akawataka waliohusika katika tukio la
juzi wachukuliwe hatua kali za kisheria na za kijeshi kwa kukiuka
maadili ya polisi. SOURCE:GPL






No comments:
Post a Comment