KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 18, 2015

APATA KIPIGO BAADA YA KUDAIWA KUUZA MISHIKAKI YA PAKA


Na Asifiwe George na Mwantum Saadi, Dar es Salaam
MUUZA mishikaki mmoja katika kituo cha daladala cha Temeke mwisho jijini Dar es Salaam maarufu kwa jina la Said Mishikaki, amekamatwa na kupigwa na wananchi kwa tuhuma za kuuza mishikaki ya nyama ya paka.
Said alikamatwa jana asubuhi baada ya taarifa kusambaa katika eneo hilo zikimtuhumu kwamba amekuwa na kawaida kuuza mishikaki ya nyama ya paka badala ya ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine wanaoliwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, baada ya taarifa hizo kuenea, wananchi walilazimika kumtafuta muuza mishikaki huyo ili wamchukulie hatua.
Baada ya kumsaka kwa dakika kadhaa, hatimaye walifanikiwa kumkamata na kumkuta akiwa na paka mmoja aliyekuwa amemchinja na kumuweka kwenye ndoo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi hao walipomuona paka huyo akiwa amechinjwa, walichachamaa na kuanza kumshushia kipigo muuza mishikaki huyo na kumuumiza sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya Kihenya, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Hata hivyo, alisema taarifa za tukio hilo zinahitaji uchunguzi zaidi ili kuzithibitisha.
“Nilikwenda eneo la tukio na kukuta kielelezo cha mfuko wa nyama hiyo. Niliona nyama na utumbo mkubwa unaoonekana kama ni wa mnyama anayekula majani mfano wa ng’ombe.Taifa Muhimbili (MNH), Dk. David Kombo alisema haina madhara yoyote kwa binadamu.
“Nyama ya paka haina madhara yoyote ya kiafya kwa binadamu, yaani binadamu hawezi kudhurika kwa kula nyama hiyo labda tu mnyama huyo awe na maradhi fulani fulani .
“Kwa kuwa nyama hiyo hailiwi katika mazingira yetu, baadhi ya watu wanapotambua wameila, wanaanza kujisikia vibaya kwa kuwa si kitu cha kawaida katika utamaduni wetu.

No comments:

Post a Comment