KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 17, 2015

CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA (CHAKUA) CHAITAKA SUMATRA KUSHUSHA NAULI ZA DALADALA NA MABASI YA MIKOANI


Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Taifa(Chakua),Hassan Mhanjama akionyesha barua kwa waandishi wa habari  (hawapo pichani) ambazo wamejibiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka).

Na Chalila Kibuda.
Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) kimesema kuwa kutokana na bei ya mafuta kushuka nchini nauli ya daladala na nauli ya mabasi mikoani inatakiwa kushuka kwa asilimia 25.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Mwenyekiti wa chama hicho,Hassan Mhanjama amesema Mamlaka ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (Sumatra) ina wajibu wa kuitisha mkutano na wadau kujadili kushuka kwa gharama ya nauli ili mwananchi aweze kunufaika bei ya kushuka kwa mafuta.
Mhanjama amesema kwa nauli ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Kilomita 10 ya sh.400 inatakikwa kushuka na kufikia sh.300 na nauli ya mkoani ya Sh.40,000 inatakiwa kushuka na kufikia sh.30,000.
Amesema kuwa wamiliki wa Daladala na mabasi ya mikoani kusema bei ya vipuli na tairi zimepanda haihusiani na kushuka kwa bei ya mafuta kwani wakati mafuta yanapanda wanalamika na bei kupandisha hivyo sasa wanalazimika kushusha nauli zao.

No comments:

Post a Comment