| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana. |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati walipokutana katika shughuli za maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyefariki jana ghafla akiwa katika Kikao cha Chama Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana kijijini kwake Makunduchi Zanzibar. |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, wakati walipokutana katika swala maalum ya kumswalia aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyefariki jana ghafla akiwa katika Kikao cha Chama Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana. |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein, wakiwaongoza baadhi ya viongozi wa Serikali na wananchi wakati wa kuswalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla jana wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana kijijini kwake Makunduchi. |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza wananchi kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla jana wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa jana kijijini kwake Makunduchi. Picha na OMR. |


No comments:
Post a Comment