KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 4, 2015

KUTOKA UTT-AMIS:ZIJUE FAIDA NONO ZA MIFUKO YA UTT-AMIS


Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS Daud Mbaga akitoa maelezo kwa Mbunge kuhusu huduma mbalimbali za UTT-AMIS mjini Dodoma hivi karibuni.

Katika makala yetu haya,Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS Daud Mbaga, anajibu swali kuhusu faida za mifuko ya UTT-AMIS 



Swali:Unaposema faida nzuri unamaanisha nini?


Jibu:Ninaposema faida nzuri namaanisha faida ambayo mwekezaji anaipata kupitia mifuko ya UTT-AMIS ukilinganisha na uwekaji au uwekazji wa namna hii yaani, uwekezaji katika masoko ya mitaji na fedha. Mfano mfuko wa umoja kwa mwaka wa fedha kufikia mwezi Juni mwaka jana ulitoa faida ya 51%. Mfuko wa Jikumu 23.82% huku ukitoa faida za bima, Mfuko wa watoto 30.82% , mfuko wa wekeza maisha 24.48% na mfuko wa ukwasi 12.2%. ikumbukwe kuwa faida inaweza kupanda au kushuka kuendana na mwendo wa soko la fedha na mitaji. Na kumbuka Mtanzania akiwekeza kupitia UTT -AMIS basi anaendelea na shughuli zake za kila siku huku UTT -AMIS ikimsimamia uwekezajia wake.

No comments:

Post a Comment