Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga
wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki
maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8
mwaka huu.(Picha zote na modewjiblog)
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara
wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara
maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu,
kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na
utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.
Nyalandu
aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga
wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki
maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata
kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
|
No comments:
Post a Comment