KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 18, 2015

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AFUNGA MAFUNZO KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI TEMEKE.

1
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5 yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Afya  kutoka Taasisi ya WAMA.

2
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke walioshiriki katika mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni. Mafunzo hayo yalifanywa na Taasisi ya WAMA ikishirikiana na Shirika la Engender Health kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, USAID.
3
Baadhi ya wanafunzi na walimu kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakiimba wimbo wa kumkaribisha mgeni rasmi alipokuwa akiingia ukumbini.                                                         

No comments:

Post a Comment