Balozi
wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka anatoa salamu zake za muungano
kwa watanzania wote na hasa wanaoishi nje ya Tanzania kwa kuwataka
watumie fursa hiyo kuimarisha utanzania wao na kuboresha maisha ya
watanzania wote hasa katika Nyanja za kisiasa na kiuchumi tunapoelekea
katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika salamu zake Mhe. Zoka amewataka watanzania wote waishio nje ya nchi kuyasoma mapendekezo ya katiba mpya kiufasaha na kwamba katika katiba hiyo wao wamepewa hadhi maalum. Ili kufanikisha utoaji wa elimu huo unafanikiwa basi Mhe. Zoka amejitolea kutoa nakala chache za katiba hiyo pendekezwa ambayo ipo katika ofisi za ubalozi mjini Ottawa kwa kila atakayetaka kupitia na kuelimisha wengine, lengo likiwa ni kuelewa kilichomo katika katiba hiyo ambayo imetayarishwa kwa kuzingatia mahitaji ya watanzania wote bila kujali mahali waliko. Aidha amewakumbusha kuwa katiba hiyo inapatikana katika tovuti ya Serikali.
Katika maswala ya kiuchumi watanzania walio nje ya nchi wameaswa kutumia fursa hiyo nzuri kujitambulisha rasmi katika balozi mbalimbali za Tanzania na kujiandikisha rasmi ili kuwekwa katika kumbukumbu za nchi hatua ambayo itaisaidia nchi kufanya makisio ya karibu ya pato la nje na kupanga malengo na mikakati ya kukuza uchumi wa nchi.

Sehemu
ya Watanzania Waishio nchini Canada wakiwa pamoja na Balozi wa Tanzania
nchini humo, Mhe. Jack Zoka wakati wa Sherehe za Muundano.Ametoa mfano
wa raia 26 wa Tanzania waliokuwa wamekumbwa na ghasia za kibaguzi
Xenophobia huko Durban SA ambao jana Serikali ya Tanzania iliwarudisha
nchini. Hatahivyo amesisitiza kuwa ni hiari ya mtu kuamua kujiandikisha
au kutojiandikisha katika ubalozi wake. Kama vile utoaji elimu hautoshi, Balozi wa Tanzania Ottawa Mhe. Jack Zoka amekosoa kwamba bado hatua za makusudi zinahitaji kuboresha jumuiya za watanzania wanaoishi nje ya nchi ili zikidhi haja za watanzania wote kwa kushirikiana na balozi husika ili kwa pamoja kuelekeza nguvu za mapambano dhini ya maadui wakuu watatu wa nchi yetu tukufu ya Tanzania ambao ni umasikini, Ujinga na Maradhi. |
No comments:
Post a Comment