KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2015

YALE YALE...ACT YA AKINA ZITTO YAANZA KUWAKA MOTO

Lucas Kadawi Limbu akisisitiza jambo
Anayejiita Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold Mahona.          
Na Dotto Mwaibale
Anayejiita Mwenyekiti  wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa ACT-Wazalendo.
Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.
“Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema Limbu Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho. “ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania. Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina lake huku msajili wa vyama akishuhudia. Alisema msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo. Limbu alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia mbaya na chama cha ATC-Tanzania.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)
      

No comments:

Post a Comment