KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 28, 2015

WABUNGE WA MADASCAR WAPIGA KURA KUMUONDOA RAIS

FILE - Madagascar's President Hery Rajaonarimampianina, May 24, 2014.
Bunge la Madagascar limepiga kura kumuondoa Rais madarakani hatua ambayo itarudisha nyuma  nchi hiyo iliyokubwa na machafuko miaka iliyopia.

Hatua ya kumuondoa Rais Hery Rajaonarimampianina iliungwa mkono na wa Bunge 121 kati ya wabunge 125 ambao walipiga kura jana.Uamuzi huo ni lazima uthibitishwe na mahakama ya katiba.

Rais Rajaonarimampianina aliingia madarakani Januari 2014 baada baada ya uchaguzi wa kidemokrasia tangu 2006. Ilitarajiwa kuwa uchaguzi huo ungemaliza mzozo wa kisiasa nchini humo baada ya mtangulizi wake Marc Ravalomanana kuondolewa kwenye mapinduzi ya mwaka 2009.

Lakini wapinzani wa Rais wanasema ameshindwa kutekeleza majukumu yake na hivyo hana budi kutoka.

Marekani, awali ilikuwa ikimuunga mkono Rais huyo, mwaka jana Marekani iliondoa vikwazo kwa nchi hiyo baada ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia

No comments:

Post a Comment