Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM
akiionyesha ilani ya uchaguzi iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya
CCM mjini Dodoma.Nape amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye
mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe
Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na
kila kijiji shilingi milioni 50 “Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani
ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo
hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM" alisema. |
No comments:
Post a Comment