KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 13, 2016

MAWASILIANO NA MOURINHO YATANIKATISHA TAMAA-VAN GAAL

Mourinho na Van Gaal katika mkutano wa hapo awali.        
Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa atakata tamaa iwapo Manchester United ilifanya mazungumzo na Jose Mourinho.
United haikutoa tamko lolote baada ya ripoti hizo za juma lililopita kwamba maafisa wa kilabu hiyo walifanya mazungumzo na wawakilishi wa aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho.
Alipoulizwa iwapo anafikiri kulikuwa na mazungumzo,Van Gaal alisema: katika soka hilo linawezekana,lakini sidhani kama kulikuwa na mazungumzo.
Amesema kuwa alikuwa na uhusiano mzuri na mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward na mmiliki Glazers na kwamba wangemwambia.
Manchester United kwa sasa hawako katika michuano ya kilabu bingwa Ulaya,na wako nafasi ya tano katika jedwali la ligi ikiwa pointi sita nyuma ya manchester City ambao wako katika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment