Waokoaji wakiwa wamebeba moja
ya miili ya watu waliokufa kwa maji mara baada ya gari aina ya Hiace
walilokuwemo katika Kivuko cha MV Kigamboni kuopolewa kutoka baharini.
Moja ya Magari ya Kikosi cha zimamoto likiwa katika eneo la tukio wakati wa uokoaji huo.
………………………………………………………………………………….
Zoezi la uokoaji Gari aina ya
Toyota Hiace lililozama baharini leo tarehe 20/04/2015 saa 10 alfajiri,
likiwa na watu wawili, limekamilika saa 12:00 jioni hii, baada ya miili
hiyo kutolewa kwenye maji na gari hilo kupatikana.
Gari hilo lililokuwa kwenye MV.
Kigamboni kutokea upande wa Magogoni kuelekea upande Kigamboni, likiwa
imeegeshwa ndani ya kivuko, ghafla lilitoka kwenye kivuko na kuzama
baharini likiwa na dereva mmoja na abiria mmoja.
Shughuli za uvushaji abiria magari na mizigo siku ya leo zimeendelea kwa vivuko vyote viwili
TEMESA inapenda kutoa wito kwa
watumiaji wa vivuko vyote kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mabaharia
wanaofanya kazi kwenye vivuko hivyo.
Uongozi wa TEMESA unatoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu walio poteza maisha.
Aidha uongozi wa TEMESA unatoa
shukrani kwa wale wote waliofanikisha zoezi la ukoaji wakiwemo; Kikosi
cha Zimamoto na Uokoaji, Kikosicha Jeshi la Wanamaji, Mamlaka ya
Bandari, Polisi Kikosi cha Maji pamoja na Viongozi mbalimbali wa
Serikali waliofika eneo la tukio




No comments:
Post a Comment