KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 28, 2016

HALI ILIVYO UWANJA WA TAIFA KUELEKEA YANGA VS MAZEMBE

IMG-20160628-WA0001
Leo pale taifa unachezwa mchezo wa kombe la shirikisho Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania Young Africans dhidi ya TP Mazembe mabingwa wa DR Congo ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu zote mbili.
Mchezo huo umekuwa na mambo mengi sana nje ya uwanja kitu ambacho kinazidi kuwafanya wadau wengi wa soka la bongo kutamani kuona na hata kujua ni nini kitatokea uwanjani ndani ya saa moja na nusu ya mchezo huo (dakika 90).
Uongozi wa Yanga umetangaza kuwa hakutakuwa na kiingilio kwenye game hiyo, sasa kilichotokea ni kufurika kwa mashabiki uwanjani kuanzia asubuhi wakianza kuingia uwanjani wakihofia kukosa nafasi itakapofika majira ya mchana.
shaffihdauda.com imezinasa picha kadhaa huku na kule na kukuletea wewe ili ujionee mwenye hali ilivyo asubuhi hii na kama una mpango wa kuushuhudia mchezo huo uwanjani basi utakuwa unajua unatakiwa kufanya nini mida hii.
IMG-20160628-WA0002

No comments:

Post a Comment