KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 27, 2016

TRUMP NA CLINTON WALUMBANA KWENYE MDAHALO MAREKANI


Trump and Clinton on stageWagombea urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi.
Kadhalika wamejibizana kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State.
Msimamizi wa mdahalo huo Lester Holt amemwuliza mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mbona kufikia sasa bado hajaweza wazi taarifa zake za ulipaji kodi.
Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amemshutumu mpinzani huyo wake akisema amekuwa akikwepa kulipa kodi na kudokeza kwamba hilo lina maana kwamba hakuwezi kuwa na wanajeshi, pesa za kulipa wanajeshi waliostaafu pamoja na kufadhili elimu na huduma ya afya.
Lakini tajiri huyo kutoka New York amejibu kwa kusema kwamba atatoa hadharani taarifa hizo iwapo Bi Clinton naye atakubali kutoa barua pepe 33,000 ambazo zilifutwa kutoka kwa sava yake wakati wa uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa kazi rasmi alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Bi Clinton amekubali lawama kuhusu kosa hilo na kusema hakuwezi kuwa na "kisingizio".
Kadhalika, Bw Trump amemlaumu mpinzani huyo wake kuhusu kupotea kwa ajira akisema nafasi za kazi "zinaikimbia nchi" na akalaumu mikataba duni ya kibiashara.
Amesema Bi Clinton amekuwa mtu wa "maneno mengi, bila vitendo".
Bi Clinton ameahidi kuongeza uwekezaji na kuahidi kuunda nafasi takriban 10 milioni za kazi.
Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo.
Kura za maoni zinaonyesha wawili hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono. BBC

No comments:

Post a Comment