ALIYEKUWA
Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor
Idrissa (wa pili kutoka kulia kwenye picha), ameteuliwa kuwa Mwenyekiti
mpya wa timu hiyo akirithi mikoba ya Alhaji Said Mohamed Abeid,
aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo, ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Idrissa. Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29 mwaka huu. |
November 29, 2016
NASSOR IDRISSA MWENYEKITI MPYA AZAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment