Diwani wa kata ya Kibindu
Ramadhani Mkufya ,akizungumza kabla ya vikundi vya ujasiriamali
vilivyopo kwenye kata yake kupatiwa hundi ya mkopo kutoka halmashauri ya
Chalinze.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Afisa vijana na maendeleo ya
jamii katika halmashauri ya Chalinze,Felister Kizito,akizungumza baada
ya kukabidhi hundi za mkopo kwa makundi mbalimbali ya ujasiriamali jimbo
hapo(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa halmashauri ya
Chalinze ,Saidi Zikatimu akizungumza na wananchi na watu waliojiunga
katika vikundi vya ujasiriamali katika kata ya kibindu.(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
………………
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
HALMASHAURI ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani imetumia kiasi cha sh.mil 79.5 ,kuwezesha vikundi 26,vya wajasiriamali wanawake na vijana katika kata mbalimbali.
Aidha halmashauri hiyo imepanga
kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali 200 kwa kipindi cha mwaka mmoja
ujao ili kuwaongezea mitaji na kuwainua kiuchumi .
Akikabidhi fedha hizo katika vikundi hivyo,mwenyekiti wa
halmashauri ya Chalinze,Saidi Zikatimu alisema ,fedha hizo zimetokana na
asilimia 10 ya mapato ya ndani ya robo mwaka kiasi cha sh.mil 809 ambayo yalikusanywa.
Alieleza kwamba upande wa kundi la wanawake wamepatiwa asilimia tano na vijana asilimia tano kati ya asilimia 10 iliyotengwa.
Zikatimu alisema lengo la kutolewa fedha hizo ni kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi ili kujiendeleza kimaisha .
“Lengo jingine ni kufuata sheria
ambayo inataka asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri yakopeshwe
makundi hayo ya vya uzalishaji mali”alisema Zikatimu.
Hata hivyo mwenyekiti huyo
alifafanua kuwa kwa kipindi hiki cha robo ya mwaka wamekusanya mil.809
katika mapato ya ndani ambapo mil.258 wametenga kwa ajili ya miradi ya
maendeleo.
Zikatimu aliwaomba wajasiliamali
hao kurejeshe fedha kwa wakati ili ziweze kuzungushwa katika makundi
mengine ambayo bado hayajapatiwa mikopo kwa kipindi hiki.
‘Mrejeshe kwa wakati fedha hizi na
mhakikishe mnazitumia kwa malengo lengwa sio tena mchezee ngoma,wanaume
muolee wake wenza ama kulewea pombe la hasha
” alisema Zikatimu.
No comments:
Post a Comment