Mabingwa watetezi
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya Yanga imethibitisha rasmi
kuachana na kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi
uwanjani,Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mkabaji
Justine Zullu toka timu ya Zesco United ya nchini Zambia.
Licha ya kuachana na klabu hiyo
mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani anaondoka kwa amani na
akiacha maneno mazito nyuma yake.
“Yanga ni kama familia kwangu
daima itabaki moyoni mwangu na kumbuka mashabiki walivyofurika kuja
kunipokea siku ambayo niliwasili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo na
ni wakati sasa wa kuwapisha vijana ili kuleta changamoto mpya ili
kuipeleka mbele zaidi klabu hii pale tulipoishia sisi”alisema Twite
Mbuyu Twite alijiunga na Yanga
msimu wa 2013-14 akicheza vyema nafasi zote za ulinzi na kusimama kama
kiungo mkabaji kwa muda mrefu na ikumbukwe usajili wake ulileta kelele
nyingi kutokana na kuwa Simba nao walitoa pesa za usajili wa mchezaji
huyu ila Yanga waliwazunguka watani zao na kumpandia dau na kuwazidi
kete.
Kiraka huyu anaondoka Yanga akiwa
na medali za ubingwa wa ligi kuu mwaka 2014-15 na 2015-16,Ngao ya Jamii
2014 na 2015 na pia atakumbukwa kwa kuweka rekodi ya kuipeleka timu
hiyo katika hatua ya makundi ya Michuano ya kombe la Shirikisho barani
Afrika.
Kumekuwa na taarifa kuwa kiungo
huyu atajiunga na mahasimu wao wakubwa nchini Tanzania timu ya Simba kwa
sasa Yanga ipo chini ya kocha mpya George Lwandamina raia wa Zambia
ambaye amechukua mikoba ya Kocha Hans Van Der Pluijm ambaye amepandishwa
cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo na kuna taarifa za chini
kuwa mshambuliaji Obrey Chirwa huenda akatolewa kwa mkopo kwenda klabu
yake ya Zamani FC Platinum na kupisha usajili wa mshambuliaji ambaye
anatajwa kuja Yanga kwa ajili ya kuimarisha kikosi katika michuano ya
klabu bingwa Afrika inayotarajiwa kuanza Februari Mwakani.
No comments:
Post a Comment