KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 21, 2017

NIT KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI

NIT
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Prof.Zacharia Mganilwa akimuonesha Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga maeneo mbalimbali ya chuo hicho wakati wa kongamano lililowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma katika chuo hicho katika miaka ya nyuma na waliomaliza mwaka ulioisha wa masomo.
NIT 2
Baadhi wa wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakiwa katika kongamano lililowakutanisha na viongozi wa chuo hicho.
NIT 3
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.Zacharia Mganilwa akiongea na wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo hicho ambapo alisema dhumuni la kuwakutanisha ni kutoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao ikiwa ni lengo la kuongeza ufaulu na kuwa na wanafunzi bora ambao wanaweza kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi kwa kutumia elimu waliyoipata kutoka chuoni hapo.
NIT 4
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga akiongea na na wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo hicho ambapo alisema taasisi yake itaendelea kuonesha nia ya kukisaidia chuo hicho ili kiendelee kukua zaidi na kutoa wahitimu bora katika soko la ajira nchini na afrika kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment