KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 22, 2017

MAASKOFU WAMUOMBEA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

DSC_0076
Mwenyekiti wa Good News For All Ministry , Askofu Dkt. Charles Gadi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji wa kazi wa Rais John Pombe Magufuli na kumshukuru kwakupiga vita uingizwaji, uuzwaji na matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini (katikati), Askofu Ernest Sumisumi wa Kanisa la Baptist, na kushoto Askofu Hezron Mwasemba wa Kanisa la Mafuta.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
1
Maaskofu wakiwa wameshika picha ya rais John Pombe  Magufuli kwa ajili ya maombezi maalumu.
2
Maaskofu wakiwa wamenyanyua picha ya rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya maombezi.
3
5
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza askofu Dkt. Charles Gadi (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza kuhusu jukumu la Rais John Pombe Magufuli kupiga vita matumizi na uuzwaji wa Madawa ya kulevya jijini Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi hasa katika zoezi gumu la kupiga vita madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa Good News For All Ministry , askofu Dkt. Charles Gadi kwa niaba ya madhehebu mbalimbali, amesema utendaji wa rais John Pombe Magufuli unapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania kwani vita ya dawa za kulevya ni kubwa na ngumu kuzizibiti lakini kwa mwenendo alioanzia mhe rais ni mzuri na atashinda vita hivyo.
Aidha askofu Dkt. Charles Gadi aliongoza jopo la maaskofu wenzake kumuombea rais Magufuli, taifa pamoja na viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment