Waziri
wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya
kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24.
Nape
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya
Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba
kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na
polisi wenye silaha.
“Matukio
kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais
yupo na nchi haijapinduliwa basi kuingia ndani ya chombo cha habari na
silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari.
"Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
"Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi
"Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya
"Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia
"Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24." Amesema Waziri Nape
No comments:
Post a Comment