KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 29, 2017

PROF.MDOE AWAHAKIKISHIA WANANCHI UMEME WA UHAKIKA

pic+focus+on+magufuli
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati Shirika la  Umeme Tanzania (Tanesco) likifanya jitihada za kufanya uchunguzi  katika mfumo mzima wa Gridi ya Taifa na kurekebisha hitilafu iliyopelekea kukosekana kwa umeme katika mikoa yote iliyounganishwa na Gridi  ya Taifa.
Profesa Mdoe aliyazungumza hayo leo katika mkutano wake na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea tukio la kukatika kwa umeme katika mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya  Taifa asubuhi majira ya saa moja
Alisema mara baada ya wataalam kutoka Tanesco kugundua hitilafu, wataalam walianza kushughulikia tatizo hilo na kufanikisha kurejesha umeme katika mikoa ya Iringa ambayo ilipata umeme saa 1:27, Dar es Salaam saa 1: 43 pamoja na Zanzibar ambayo ilipata umeme saa 2: 42 na kuongeza kuwa ilipofika saa 2:50 mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya Taifa ilipata umeme.
Alieleza kuwa uwashaji wa mitambo unaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha hitilafu bado unaendelea.
Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi katika Masuala ya Usafirishaji Umeme Mhandisi Kahitwa Bishaija alisema mpaka sasa tatizo limeshadhibitiwa

No comments:

Post a Comment