KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 29, 2017

WANANCHI BINAFSI WANAWEZA KUKOPA (MOGEJI) MORTGAGE MOJA KWA MOJA KWENYE MABENKI:MTAALAMU BoT

C
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WANANCHI
binafsi wanaweza kwenda kwenye mabenki na kuomba mikopo ya fedha za ujenzi, (Mortgage
Finance), bila ya kuanza kupitia kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi-Usimamizi wa Mabenki  Benki Kuu ya Tanzania, (BoT),  Bw. Eliamringi Mandari, (pichani juu), wakati
akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa mikopo ya fedha kwa ajili ya ujenzi,
(Mortgage Finance) na utunzaji taarifa mteja (mkopaji) katika kitunza taarifa
cha kibenki, (Databank) kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha
leo Machi 29, 2017 inayoendelea kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (tawi la
Zanzibar), mjini Unguja.
“Watu
wengi hawajui kama kuna fursa hii ya ku-mortgage, kwa maana ya kujenga, kununua
au kurekebisha nyumba yako, na katika kudhamiria kufanya hayo, benki inaweza
kutoa masharti ambayo ni ya kurejesha fedha (mkopo) huo kwa muda mrefu kati ya
miaka 5 hadi 20.” Alisema.
Hata
hivyo alisema kama ilivyo kwa masharti mengine yahusuyo kukopa, hata fursa hii
ya kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi vigezo na masharti pia huzingatiwa ili
benki iweze kutoa mkopo huo.
Aidha
kuhusu mfumo wa taarifa unaosaidia mkopeshaji,(lender), kumjua mkopaji,
(borrower), ujulikanao kama, Credit
Reference System, (DBS), alisema Sheria namba 48 ya BoT kuhusu masuala ya
kubadilishana taarifa za mikopo, kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha inalazimisha
mabenki na taasisi hizo kutuma taarifa za wateja (wakopaji), kwenye Databank ya
BoT kila mwezi, alisema Bw. Mandari
Alisema pia BoT, inaandaa utaratibu
utakaolazimisha wakopeshaji binafsi na Taasisi za Kibinafsi, (NGOs),
zinazojihusisha na utoaji mikopo, kusimamiwa, (Regulated), katika utoaji wa
taarifa za mteja (mkopaji), katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank), ili
kuwaondolea usumbufu wananchi.
 “Ni kweli Sheria  inaitaka Benki Kuu kusimamia taasisi za fedha
zinazochukua amana kutoka kwa wananchi, kwa kuwasilisha taarifa hizo za
wakopaji kwenye mfumo huo wa BoT wa Databank, lakini kwa sasa wakopaji binafsi
na taasisi za hiari zinazojishughulisha na utoaji mikopo ya kifedha, bado sera
inaandaliwa ili na wao waweze kusimamiwa.” Alisema.
Alisema,
wakopaji binafsi na NGOs zinazojihusisha na utoaji mikopo, zimekuwa zikitumia
mabavu wakati mwingine katika kufuatilia marejesho ya mikopo kutokana na
utaratibu usio wazi wa kukopa, na wakati mwingine wakopaji wanarejesha mikopo
kwa riba kubwa, alifafanua.
 Bw. Eliamringi Mandari, akiwasilisha mada hiyo
Meneja Msaidizi Msoko ya Ndani wa BoT, Bw.Genes Kimaro,  akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa Sera ya Fedha wa BoT.
 Bw.Genes Kimaro
 Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa BoT, Bw.Mohammed Kailwa, (kushoto), akijibu baadhi ya hoja wakati akisaidiana na Meneja wa Masoko ya Ndani, Kurugenzi ya Masoko ya Fedha (BoT), Bw.Reverian Felix

No comments:

Post a Comment