Kamati ya Uchaguzi ya Chama
cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA), leo Juni 16, 2017 imetangaza rasmi
Uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka
huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa
10.00 jioni. Ratiba kamili kuelekea uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-
Juni 23, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.
Juni 24, 2017- Kamati ya
Uchaguzi kutangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza
taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba
au kanuni za TWFA.
Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
Juni 29, 2017- Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
Juni 30, 2017- Usaili kwa wagombea waliotangazwa
Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
Julai 03, 2017- Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa
Julai 04, 2017 Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Julai 04 hadi 07, 2017-Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili
Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA
Mushumba amesema kwamba nafasi
zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne
wa Kamati ya Utendaji. Sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha
nne.
Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh
200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na
Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000.
Fomu zitapatikana ofisi za Hosteli ya TFF zilizoko Karume, Ilala jijini
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment