KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 21, 2017

WAKILI WA TUNDU LISSU AELEZWA KWANINI MTEJA WAKE ALIKOSA DHAMANA

Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Karume amesema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema

Amesema hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu.

Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika.

Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

“Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa.

No comments:

Post a Comment