Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewashukuru viongozi wote wa
Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za Kidini vyombo vya habari na
watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke wake Bibi Linah
Mwakyembe uliotokea Julai 15 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Misa ya
mazishi ya mke wake huyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Kyela Mhe.
Mwakyembe ameeleza kuwa amefarijika sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila
mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki kigumu na kuahidi kuendelea
kushirikiana nao katika kila jambo.
“Mimi na wanangu tumefarijika
sana kwa kuona jinsi ambavyo Watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na
upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na mmetuoshesha
ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi Mungu awabariki
sana na asanteni sana”Alisema Mhe Waziri Mwakyembe.
Kwa Upande wake Mhe.Amos Makala
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati akitoa salamu za pole kwa niaba ya wanachi
wa mkoa wake amesema wananchi wa Mbeya watamkumbuka marehemu mama Linah
Mwakyembe kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia jamii katika mambo
mbalimbali ikiwemo kufundisha jamii kumcha Mungu pamoja na
Ujasiriliamali uliosaidia wanawake wa Kyela kujiajiri.
“Wananchi wa Mbeya tunakupa pole
sana Mhe. Mwakyembe pamoja na familia yako lakini pia tunamshukuru
Mwenyezi Mungu kwa maisha ya mama Linah hapa duniani ambayo yameleta
faida kwa jamii tunamuomba mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi
amina lakini na wewe pia tunakuombea Mungu aendelee kukupa uvumilivu na
uamini kuwa hili nalo litapita”.Alisema Mhe Makala.
Marehemu Bibi Linah Mwakyembe ameagwa na kuzikwa jana nyumbani kwake Kyela na ameacha watoto watatu.
No comments:
Post a Comment