KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 27, 2017

ZITTO AWAJIBU WANAOMKOSOA KWA KUMPONGEZA RAIS DKT.MAGUFULI

 Na Regina Mkonde
 Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewajibu baadhi ya watu wanaomkosoa na kumuita msaliti kutokana na kitendo cha kumsifia Rais John Magufuli alipokuwa ziarani jimboni humo.

Zitto alijibu mapigo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kigoma Mjini, ambapo alisema asingeweza kumkosoa Rais Magufuli wakati ule kwa kuwa alikuwa mgeni jimboni kwake, pia alikuwa anafanya shughuli za maendeleo ya wananchi wa jimboni kwake.

“Rais alikuja hapa akafungua mradi wa maji tukaenda ziwa Tanganyika, kuna watu walikasirika sababu Rais alinisifia sana, hawezi akaja Kigoma mtu akanisema mimi vibaya msingekubali, na mgeni akija siwezi nikaanza kumsema vibaya, mgeni akija unamkaribisha anafanya kazi yake anaondoka, kwani rais akienda kwenye majimbo yao wanamsema, rais alikwenda Bukoba Mjini wakati wa tetemeko, mbunge wa jimbo hilo alimsema ? alikwenda Arumeru kwa mdogo wangu Joshua Nasari, alimsema rais kwa nini akija kigoma mimi ndio nimseme,” alihoji Zitto.

Aliongeza kuwa “Mimi hamkunifundisha kuwa mazwazwa wazee mlinifundisha adabu na kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini sio kwamba rais akikosea hatutamsema tutamsema, na tumeshamsema sana, sisi ndio chama cha mwisho kufanya mkutano wa ziara, tukaja operesheni ya linda demokrasia tumemaliza mikutano ikapigwa marufuku.”

“Lakini toka serikali ya awamu ya tano iingie madarakani uhuru umeanza kuminywa sasa ni lazima, hatuwezi kukaa kimya haki ya watu kuwa na mawazo tofauti hatuwezi kuikalia kimya hata kidogo, lakini wakati huo huo hatuwezi tukasimamisha kila kitu kusubiri haki ya kuwa na mawazo huru, lazima haki ya mawazo huru ipiganiwe wakati tunapigania maendeleo,” amesema

No comments:

Post a Comment