KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 21, 2017

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA-SIMBA VS MBAO KIRUMBA

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Alhamisi Septemba 21, 2017 kwa mchezo mmoja utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Katika mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 10.00 jioni utakutanisha timu za Mbao FC ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam.
Utakuwa ni mchezo pekee kwa siku ya kesho Alhamisi kabla ya ligi hiyo kuendelea Jumamosi ambayo kutakuwa na michezo minne ambako Young Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Michezo mingine itakuwa ni Singida United itaialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui ilihali Majimaji itakuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Jumapili Septemba 24, mwaka huu kutakuwa na michezo mitatu ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Wakati mechi zote hizo hapo juu zikianza saa 10.00 jioni, mchezo mwingine siku ya Jumapili utaanza saa 1.00 jioni kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi ukikutanisha Azam na Lipuli ya Iringa.

No comments:

Post a Comment