Timu ya Mbao FC imekuwa ya kwanza
kuifunga Simba magoli mawili tangu msimu uanze kwani imeweza kucheza
mechi tatu bila kuruhusu nyavu kutikiswa Mchezo uliomalizika kwenye
uwanja wa CCM Kirumba kwa kutoka sare ya 2-2 Mzunguko wa nne wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara .
Simba walimudu kucheza mechi tatu
bila kuruhusu bao katika nyavu zao huku Aishi Manula akiwa amecheza kwa
zaidi ya dakika 325 bila kufungwa.
Hii imekuwa ya pili kwa Simba huku
ikiwa ya kwanza kwa Mbao FC baada ya kucheza mechi nne ,ikishinda
moja,sare moja na kufungwa Miwili huku Vijana wa Omog wakishinda mechi
mbili na kutoka sare mbili.
Mchezo uliochezeshwa na refa
Athumani Lazi wa Morogoro, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao
1-0, lililofungwa na winga machachari, Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya
16 akimalizia krosi nzuri ya beki Erasto Edward Nyoni.
Kichuya alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 44 baada ya
kuumia na kumpisha Haruna Niyozima, wakati Mbao nalo walimtoa Said Said
dakika ya 37 na kumuingza Herbet Lukindo.
Kipindi cha pili Mbao walirudi kwa kasi nzuri na kufanikiwa
kusawazisha bao dakika ya 46 tu, kupitia kw3a Habib Kiyombo ambaye hilo
linakuwa bao lake la tatu msimu huu.
Hata hivyo, Simba walijibu kwa mashambulizi mfululizo na
kufanikiwa kupata bao la pili dakika tatu baadaye, mfungaji kiungo
Mghana, James Kotei.
Mbao hawakukata tamaa, waliendelea kushambulia na kufanikiwa
kusawazisha tena dakika ya 81 kupitia Emmanuel Mvuyekire aliyefunga kwa
shuti la mbali pia.
Hadi mwamuzi anamaliza Mpira timu hizo zimeweza kugawana alama
huku Simba wakibaki kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 8 na Mbao Fc
wamefikisha jumla ya Pointi 4,Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea wikendi hii
na kinara bado anaongoza Mtibwa Sugar wenye pointi 9 ambao hawajapoteza
hata mechi moja .
No comments:
Post a Comment