KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 18, 2017

UJUMBE WA WATSUP WAMPONZA MBUNGE

Mbunge mmoja nchini Kenya ametakiwa kuomba radhi mara baada ya kutuma ujumbe wa kimapenzi kwenye group la Whatsapp la wabunge.

Anthony Kiai alituma ujumbe wa kimapenzi kwenye group na kuwaomba wabunge wenzake kutoutilia maanani kwani amekosea lakini wabunge wenzie katika group hilo walimtaka kuomba radhi.

Aidha, Admin wa group hilo, Bernad Chege, alimuomba mbunge huyo kuomba radhi, na badala yake msaidizi wa Mbunge huyo ndio akaomba radhi kwa kitendo hicho cha bosi wake kutuma ujumbe wa mapenzi katika group hilo

Ujumbe huo ulioandikwa kwa lugha ya Gikuyu ambayo inaongelewa na Wakikuyu nchini Kenya, ilikuwa ikitoa maelezo jinsi ya kumridhisha mwanamke chumbani, huku baadhi ya wabunge wengine walionekana kumtetea wakisema ngono sio dhambi.

Hata hivyo, Mbunge Kiai amekuwa mbunge wa jimbo la Mukurweini kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Agosti 8, 2017

No comments:

Post a Comment