KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 17, 2017

KAMA ULISHIRIKI KUSAMBAZA UJUMBE HUU BASI IMEKULA KWAKO

Hatimaye, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekanusha juu ya taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa zikiwahusu vigogo wa shirikisho hilo wakiongozwa na rais wao, Wallace Karia kujilipa posho ya kiwango cha juu.
 
Hivi karibuni kulisambaa taarifa mitandaoni juu ya vigogo hao wa TFF kujilipa fedha nyingi.

Kumbuka viongozi wa kuchaguliwa TFF hawapati mishahara, badala yake wanalipwa posho, sasa ilielezwa kwamba Karia analipwa Sh milioni sita, makamu wake Sh milioni tano huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakilipwa milioni moja kwa kila mwezi.
 
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema suala hilo halina ukweli na kudai kuwa Karia alikataa kulipwa na kusisitiza posho yake ipelekwe katika masuala mingine ya kimpira kwa kuwa yeye ni muajiriwa serikalini na analipwa mshahara huko.
 
“Hizo taarifa hazina ukweli wowote kwa sababu viongozi wa hapa hakuna ambaye anachukua kiasi hicho cha fedha.
“Hata kwenye suala la wajumbe, nao hakuna ambaye anapokea shilingi milioni moja kwa mwezi kama inavyosemekana badala yake tunatoa shilingi milioni moja na nusu kwa miezi mitatu tena kwa yule ambaye anachakarika na tunaona juhudi zake kwa kupitia ripoti ambazo anawasilisha kwenye vikao.
 
“Lakini kwa sababu jambo hilo limechafua sura ya taasisi yetu tuna mpango wa kuwafungulia kesi ya makosa ya kimtandao wale wote ambao wamehusika kwenye suala hilo na tayari tuna majina 10 ya watu ambao tutaanza nao,” alisema Kidau.

Pamoja na TFF kuamua kulitolea ufafanuzi suala hilo, bado inaonekana haukuwa mjadala mpana hasa nje ya mitandao na huenda waliamua kuwahi mapema ili kumaliza mjadala.
 
WARAKA WA TUHUMA UNAZOSAMBAZWA NI HUU;

“KAMATI TENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) KUTUMIA MILIONI 438 KWA MWAKA  KUJILIPA POSHO.
Tarehe 28/10/2017 Kamati ya Utendaji ya TFF, ilifanya Kikao katika Hoteli ya SEA SCAPE Kunduchi Beach jijiji Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine ilipitisha azimio la Wajumbe wa Kamati hiyo kuanza kulipwa posho  ya kila mwezi kwa mchanganuo ufuatao: 
 
1. Rais wa  TFF  Tsh.Mil.6 kwa mwezi  sawa na Mil.72 kwa Mwaka.
2. Makamu wa Rais wa TFF, Tsh. mil. 5  kwa mwezi sawa na Mil.60 kwa mwaka.
3. Wajumbe 20 wa Kamati ya Utendaji kila mmoja Tsh. Mil. 1 kwa mwezi sawa na mil.12 kwa mwaka ,  kwa wajumbe 20 ni Tsh.  Mil. 240 kwa mwaka.
 
NB: Posho hizi ni mpya na hazijawahi kuwepo katika shirikisho hilo katika uongozi uliopita.  
 
Aidha Posho za kila kikao zimepanda kutoka Tsh. 300, 000/=  uongozi uliopita hadi laki tano (500,000/) uongozi wa sasa kwa kila mjumbe,  kwa mwaka kuna vikao vya kawaida visivyopungua sita,  kwa Wajumbe wote 22 kwa mwaka itakuwa mil.66. 
 
Kwa  mchanganuo huo, Gharama za Posho tu kwa mwaka kwa Wajumbe wa  Kamati ya Utendaji tu ni milioni mia nne thelathini na nane (mil.438). Bado posho za vikao vya dharura, posho za watumishi wengine n.k
 
Moja ya changamoto za maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania ni Ukosefu wa fedha.  Timu zetu za taifa zinashindwa kukaa kambini,  Waamuzi wanakosa Mafunzo, viwanja vya michezo vinashindwa kuboreshwa, vilabu vya michezo havisaidiwi na mambo mengine chungu nzima hayafanyiki sababu ya ukosefu wa fedha, leo hii EXCOM  inakwenda kujifungia Sea ESCAPE na kuidhinisha  mil. 438 kwa ajili kujilipa posho!  

Kwa mwendo huu tusitegemee maendeleo katika soka Tanzania. Rais wa TFF,  WALES KARIA na Makamu wake, MICHAEL WAMBURA wanapaswa kujitathmini upya,”.

No comments:

Post a Comment