KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 19, 2018

KESI YA UHUJUMU UCHUMI YA VIGOGO WATATU WA SIX TELECOMS YAPIGWA KALENDA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeipiga kalenda kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga na wenzake kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Mbali na Dk. Tenga, washitakiwa wengine ni Mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Wakili wa Serikali, Leonard Challo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, inadaiwa kati ya January 1, 2014 na January 14,2016 Dar es Salaam washitakiwa, walitoza malipo ya simu za kimataifa kwa kiwango cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa katika tarehe hizo, washtakiwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,736,861, sawa na Sh bilioni nane
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcMj5Ie5RxZOFEsxcb3NALERYMvp6nmty-K9x76VDkEN1E-ROuhqGyulI9TlW-6oa5AGCj4R4XqIb6MkAY1HDzjqy3Ongl8Vw0PikbmbqnbW7M71g3fPB6OfGYwR5CuLu1s-_zyCcX5rr1/s1600/index.jpg
Pichani ni Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo hao Watatu wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga na wenzake wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo .

No comments:

Post a Comment