KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 19, 2018

KILIMANJARO MARATHON 2018 YAZINDULIWA RASMI MOSHI

Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambayo ni ya 16 tangu kuanzishwa kwake, imezinduliwa rasmi Kibo Palace Homes kwa kushirikisha wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA) na waandaaji wa mbio hizo.

Akizindua mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri kwani wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu kabisa tangu kuanishwa kwake miaka 16 iliyopita na hivi kufanya Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla ifahamike na watu kutaka kupatembelea. 

Mkuu wa Mkoa huyo alitoa wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizurikwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti kutokana na wingi wa watu huku pia akiwataka washiriki hasa wanaotokea Kilimanjaro kuonesha mfanomzurikwa kushinda zawadi nyingi iwezekanavyo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3ipXsJOftU0NbujkzuS2rskUbL9JKbPtAw0IfjuIa2tSBJHUmR_9rXGeNtZAdT01l2-4alK_0Ctll-j8j6FEGeFIrPtro07vnRr5cm6WIaTW9GBi2ZWKsN9HC-_HlOTMVhl8osJzinDQ/s1600/uzinduzi+%25281%2529.jpg
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akizindua Kili Marathon 2018 Kibo Palace Homes Moshi huku akiwa na viongozi na wadhamini wa mbio hizo.
 

“Ofisi yangu iko tayari kabisa kushirikiana na nyinyi na kuwa mwenyeji wa tukio hili muhimu kwani tutahakikisha kuna usalama wa kutosha ili washiriki wawe salama na amani wakati wote wa mashindano,” alisema huku pia akitoa raikwa washiriki kuhakikisha wanatembelea vivutio mbalimbali vya utalii ndani na nje ya Kilimanjaro baada yam bio hizo. 

Alipongeza wadhamini wengine wakiwemo First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum, AAR ambao ndio wabia rasmi wa matibabu, Kibo Palace Hotel iliyodhamini uzinduzi huo na waandaaji Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions ambao ni waratibu wa kitaifa. 

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7I0BcJ6SJ4AJCdQowBC-7qwRxY8hoXjv3lo5_8p2BoOSAWTfOGg5aa1kcoEYTb2K0cjwram8Uti3hLU0GTHxDM_c4a5dNNVhKMg9V2YC8BWx7ZYrcW6XBe7GrJxWlh91kUfM_OoxzIZI/s1600/kavishe.jpg
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni wa TBL Group (Afrika Mashariki, George Kavishe alisema Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 16 sasa kutokana na weledi na uzoefu mkubwa wa waandaaji ambao wamefanya mbio hizoziwe maarufu sana na moja ya matokeo makubwa nchini. Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni wa TBL Group (Afrika Mashariki, George Kavishe akizungumza katika uzinduzi huo.

Alisema kwa mwaka huu, Kilimanjaro Premium Lager imejiandaa vizuri kwani itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh milioni 20 ambapo mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 42 kwa upande wa mshiriki mwanaume na mwanamke watapata tsh milioni 4 kila mmoja. Alisema mbio maarufu zakilometa 5 maarufu kama Fun Run, zinazodhaminiwa na Grand Malt pia zitafanyika ambapo watu wa rika zote wanaruhusiwa kushiriki. 

“Hizi ni mbio za kujifurahisha kwa hivyo watu wa rika zote wanakaribishwa kushiriki ili pia iwe kama sehemmu ya mazoezi huku wakipata kinywaji chao cha Grand malt chenye afya tele,” alisema. Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza kwenye uzinduzi wa hafla hiyo.

http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2018/01/Tigo.jpg
Kaimu Mkurueni wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema wamejiandaa vizuri kwa kilometa 21 na kuwataka washiriki wajiandikishe kwa wakati kwani mbio hizo zimekuwa maarufu sana na hii imewapasababu zaidi ya kuendelea kudhamini mbio hizo. 
 

Alisema katika mwaka wake wan ne wa udhamini, Tigo itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh Milioni 11 ambapo washindi wa kwanza hadi 10 watapata zawadi huku wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake akipata Milioni 2 kila mmoja na kuongeza kuwa washiriki wote watakaomaliza mbio hizo watapata medali.

  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzPaKU5njkhQt4fTq6Qa-OE0oJYChXk7uSWw2P04A1rLecFboRnFJdGNLPm3GwdV3fj3EM5p82wJCNO7voFDE8YPThBvhbFhaMli4cgaI3GK9RpCtoTXUKVyrwZPgDmOM9TZWdp6ru4oY/s1600/Pamoja.jpg
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akiwa na wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers ambaye pia ni Muandaaji wa mbio hizo, John Addison alisema maandalizi yote yamekamilika na mbio za mwaka huu zitafanyika katika Machi 4 katika Chuo Cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42 zinatarajiwa kuanza. “Tunawashukuru mno wadhamini wetu kwa kutuunga mkono kwani tunatarajia kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa makubwa na ya kusisimua zaidi,” alisema.

No comments:

Post a Comment