KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 19, 2018

WAKULIMA WA USAGALI AMCOS WILAYANI NZEGA WAMUOMBA MKUU WA MKOA KUWASAIDIA ILI WALIPWE DENI LAO LA MILIONI 193

RS TABORA

WAKULIMA wa Tumbaku wa Chama cha Msingi cha Ushirika Usagali (AMCOS) wilayani Nzega wameiomba Serikali ya Mkoa wa Tabora kuwasaidia kusimamia madai yao ya fedha zao kiasi cha shilingi milioni 193 za mauzo ya tumbaku kwa msimu 2015/2016 ambayo watuhumu kuchukuliwa na viongozi waliokuwa madarakani wakati huo.

Wakulima hao walitoa kilio hicho jana katika Kijiji cha Usagali wilayani Nzega wakati Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey akiwa katika ziara ya kutembelea Vyama vya Ushirika kuhimiza upandaji miti kupitia ushirika kwa ajili ya kurudisha uoto wa asili na kukifanya kilimo cha tumambaku kiwe rafiki kwa mazingira.

Mmoja wa wakulima Peter Mashoto alisema kuwa waliokuwa Viongozi wa Usagali na wajumbe wa Bodi wanatuhumiwa kulipwa fedha na Kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) lakini wao walishindwa kuwalipa wakulima waliouza tumbaku yao na kuzichua wao kwa ajili ya matumizi binafsi.

Aliongeza kuwa wakulima waliodhulumiwa fedha hizo wameendelea kuishi maisha ya dhiki wakati watuhumiwa wanaendelea kuishi maisha mazuri na kujiendeleza wao binafsi huku wao wakishinda hata kuwaeneleza watoto wao kielimu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa sasa wa Usagali AMCOS Alphonce Sylvester aliomba Mrajisi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuwasaidia kusimamia madai ya wakulima ili waweze kulipa fedha zao na kuwarudishia matumini.

Alisema kuwa baadhi ya wakulima wanaolima zao hilo yamekata tamaa baada ya kuona fedha za msimu msimu 2015/2016 hawajalipwa na kuona kuwa vitendo vya namna hiyo vinaweza kuendelea.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUbUxkthlMyGtWHI31yud9fwMk6mZOczmoxqP-TJLv-E68m-DiYSKqpPnSv05njB41p4UKyPD8Ssbl7hyaLO18b0DqYMAtmn5WU7GRLVmFThnkIw5OYHdViJLbNFzLgKqf3Gpecd3il0gc/s1600/DSCN0161-750x375.jpg
Sylvester aliongeza kuwa ili kurudisha matumaini kwa wakulima ni vema Serikali isaidie kusimamia ili haki itoewe na wakulima waweze kupata fedha zao.Kufuatia kilio hicho cha wakulima hao, Mkuu wa Tabora Mwanri aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kwa kushirikiana na Ofisi ya Mrajisiri Mkoa kufuatilia suala hilo na kuoana limekwamia wapi ili wakulima waweze kupatiwa haki yao kama madai yao ni halali.

Aliongeza kuwa ni jukumu lao kuhakikisha wanawashika mkono wakulima walidhulumiwa ili hatua dhidi wahusika zichukuliwe kwa ajili ya kuhakikisha haki inatendeka.Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Jacob Ntalitinya aliahaidi kushirikiana na viongozi wa Ushirika kushughulikia tatizo hilo lilikwamia wapi ili wakulima wapate fedha zao na wahusika wachukuliwe hatua zinazostahili.

No comments:

Post a Comment