KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 20, 2018

EQUITY YAZINDUA APP KWA WATEJA WAKE

Benki ya Equity Tanzania imezindua programu tumishi (app) ya EazzyBanking ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za kibenki popote walipo hata kama hawajatembea na kadi za ATM.
Akizungumza kuhusu programu hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Joseph Iha alisema app ya EazzyBanking imeanzishwa ili kuwarahihsishia upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo ambazo zilikuwa hazipatikani awali.
Iha alisema kabla ya kuaznishwa kwa programu hiyo, walizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo kuhusu huduma ambazo wangependa ziboreshwe ili kuwarahisishia wao kupata huduma kwa urahisi, ambapo katika hilo baadhi ya huduma ambazo wateja kwao waliona ni kero zilipunguzwa na zingine zikaanzishwa ikiwepo app ya EazzyBanking.
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Joseph Iha akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu tumishi (app) ya EazzyBanking uliofanyika katika hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
“Equity tunapenda kufatilia kwa wateja wetu ni mambo gani wanapenda yaboreshwe ili kuondoa usumbufu katika utaratibu mzima wa utolewaji huduma, hivyo tuliamua kuanzisha EazzyBanking ili kurahishisha mfumo mzima wa uendeshaji wa akaunti na utoaji wa huduma, pili ni usalama wa pesa lakini tatu kuondoa usumbufu ili muda wowote, sehemu yoyote uweze kutumia pesa yako,
“Huduma nyingi ambazo yanawafanya kwenda kwa wakala ndiyo zimewekwa kwenye hiyo app kama kununua salio, kulipa bili kama za umeme na kama upo kwenye supermarket au kituo cha mafuta usihangaike, kupitia app hii unaweza kufanya malipo bila tatizo lolote, pia unaweza kutoa pesa kwa wakala hata kama huna kadi ya ATM,” alisema Iha.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kupitia app hiyo, wateja wataweza kukopa pesa muda wowote kati ya Tsh. 10,000 na Tsh. 3,000,000 na riba ya huduma hiyo itakuwa kati ya asilimia 2 hadi 10, na hiyo inatokana na matumizi ya app hiyo ya mteja mwenyewe.
Aidha alisema pamoja na hilo benki imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma zake ambapo kwa sasa ipo katika nchi sita barani Afrika na kwa hapa nchini wana matawi 15 na mawakala karibu 1,600.

No comments:

Post a Comment