Mbunge
wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ameitaka serikali iiondoe bungeni
Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2018/19, kwa sababu imejaa
kasoro zinazotakiwa kurekebishwa kabla haijapitishwa.
Amesema
bajeti hiyo inatakiwa kurekebishwa kabla haijapitishwa kama ilivyo
kawaida ya wabunge kupitisha bajeti zenye kasoro kama ilivyofanyika juzi
katika bajeti ya Wizara ya Kilimo iliyokuwa na kasoro mbalimbali.
Bashe
ameyasema hayo bungeni leo Mei 18, alipokuwa akichangia bajeti ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2018/19 iliyowasilishwa juzi na
Waziri wa Wizara hiyo, Luhaga Mpina.
Amesema hoja za baadhi ya wabunge zinazohusu maisha ya wananchi zinafia katika vikao vya vyama vya siasa.
“Naweza
kuonekana mbaya kila ninapokuwa nikiikosoa serikali lakini nitaendelea
kusema ukweli kwa kuwa nilianza kuwa na kadi ya CCM kabla sijawa
mbunge,” amesema Bashe.
Bashe
alieleza jinsi Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alivyowahi kuitwa na Kamati
ya Bunge ya Uongozi baada ya kutaka kuwasilisha hoja ambayo
haikuwafurahisha baadhi ya watu.
No comments:
Post a Comment