KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 18, 2018

BULEMBO: MPINA ANA MPANGO WA KUIONDOA CCM MADARAKANI


SeeBait
Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), amesema Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ana mpango maalumu wa kuiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19, Bulembo amesema kama operesheni sangara inayofanyika katika Ziwa Victoria ikiendelea CCM itakuwa na wakati mgumu wa kuwaomba kura wananchi katika Uchaguzi Mkuu na Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwakani.

“Kuna haja operesheni hiyo isimame ili kuwaokoa wavuvi ambao wanaathiriwa na operesheni hiyo,” amsema Bulembo.

Bulembo amemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuunda Tume ya kwenda kuchunguza operesheni hiyo kwani wavuvi wanaishi nchini kama watumwa.

 “Wizara hii kwa kweli tuna majonzi sana, nashukuru Mheshimiwa Spika umekaa hapo mbele, ni vyema ukaunda tume ya Bunge kwenda kuangalia matatizo na madhara yaliyowakuta wafugaji na wavuvi.”

Bulembo akichangia kwa hisia  amesema: “Wavuvi wa Tanzania wako katika utumwa kwa sababu ukienda Ukerewe (anataja na visiwa mbalimbali)  maisha yao ni uvuvi, hawa watu leo ni kilio, si kilio kidogo ni kikubwa, watu wamejinyonga, wamepigwa risasi.

“Wana CCM wenzenu, tutakwenda kuomba kura, tutakwendaje kuomba kura, haiwezekani utu wa mtu ukaharibika kwa sababu Mpina ni waziri, katika hili tume haipukiki, CCM ni ya watu, Rais anaongelea wanyonge, wanyonge wa Mafia, Mtwara, kanda ya ziwa.

“Mnakwendaje kuomba, Mtanzania anakuwa mtumwa, wafanyakazi wanalia, wakulima wanalia, itawezekanaje, Mpina huwatendei haki.”

No comments:

Post a Comment