Mbunge
wa Itilima, Njalu Silanga (CCM), amehoji ng’ombe 339 katika Jimbo lake
kuendelea kushikiliwa na Serikali wakati mahakama iliamuru waachiwe
huru.
Akichangia
bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Silanga amesema wafugaji
wameteseka hususani wa kando kando ya hifadhi huku akitaka miundombinu
katika minada iboreshwe ili iwasaidie wafugaji kusafirisha mifugo.
“Kwenye
Wilaya yangu ya Itilima ng’ombe 339 wa wafugaji wanashikiliwa na
serikali waKati mahakama iliamuru waachiwe, mambo haya yapo kisheria
lakini tunadhulumiwa baadhi ya vyombo vinazuia ng’ombe zetu Waziri
tusaidie kwanini jambo hili linaendelea.
“Ukiachilia
mbali suala la ng’ombe, katika maeneo yetu hatuna miundombinu mizuri
nia yetu ni ya dhati lakini lazima msaidie wafugaji lakini pia
nikupongeze Waziri kwa mipango yako ya kuhakikisha Kiwanda cha Shinyanga
kinafanya kazi,” amesema Silanga.
No comments:
Post a Comment