Mbunge
wa Serengeti, Marwa Chacha (Chadema) amedai Wizara ya Mifugo na Uvuvi
ni Wizara hewa ambapo pia amehoji ni kwanini Serikali imekuwa
ikiwanyanyasa wavuvi kwa kuwanyang’anya nyavu zao.
Akichangia
bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi bungeni jijini Dodoma jana Mei 17,
wizara hiyo ilitengewa fedha za maendeleo Sh bilioni nne lakini hakuna
fedha waliyopewa.
“Najiuliza
kwanini wameiweka hii wizara peke yake na kuitenganisha na Kilimo au
ilikuwa kuwatafutia ‘washkaji’ ulaji, maana yake ni kwamba hamtaki
kusikia biashara ya wavuvi nchi hii.
“Ng’ombe 300 wamepigwa mnada ila tembo akila shamba la ekari tano mhusika analipishwa faini ya Sh 100,000 kwa ng’ombe mmoja.
“Wafugaji
wetu wanapata shida mtapata hela wapi Ulega (Abdallah, Naibu Waziri wa
Kilimo) mwaka uliopita hamkupewa hata 100 afadhali mje hata mimi naweza
kuwafadhili,” amesema Marwa.
No comments:
Post a Comment