Na Mwandishi Wetu,Mbeya
Serikali imeendelea kuwasisitiza waajiri wote
nchini kuwapeleka watumishi
wao Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)
kupigwa ‘msasa’ namna ya kufanya kazi za utumishi wa umma.
Akizungumza jijini hapa mwishoni wa wiki wakati wa Mahafali ya 28
ya TPSC Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika alisema kuwa ni muhimu waajiri hao
wakawapeleka watumishi chuoni hapa hasa ikitiliwa maanani kwamba TPSC ndiyo
chuo kilichopewa dhamana ya kuendesha mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiri
wapya wa serikali.
Alisema pamoja na makujuku hayo pia Chuo hicho
kina wajibu wa kusimamia mitihani ya utumishi wa umma katika program ya
kuendeleza watumishi.
Pia TPSC inatoa mafunzo ya kozi nyingine za muda
mrefu na mfupi katika maeneo ya uongozi, Utawala na ya matumizi ya mifumo ya
kisasa ya TEHAMA.
Waziri Mkuchika aliwaasa wahitimu kwamba mafunzo
waliyoyapata chuoni hapo yasiishie kwenye vyeti bali yawe ni mafunzo ya kufanya
kazi kwa weledi na kasi mpya yenye ufanisi wa ili kuleta tija kwa lengo kukuza
uchumi wa taifa hili.
“Ninawasihi huu usiwe mwisho wa kujiendeleza kwani
mafunzo huongeza ujuzi , weledi na mbinu maridhawa za ufanisi wa kazi hususan katika
kujifunza teknolojia mpya,” alisema.
Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika akizungumza
mwishoni mwa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC chuoni hapo Jijini Mbeya.
|
Mtendaji Mkuu wa TPSC Dkt Henry Mambo akizungumza wakati wa Mahafali hayo ya 28 ya TPSC Jijini Mbeya |
Baadhi ya wafanyakazi wa TPSC wakifatilia mahafali hayo |
No comments:
Post a Comment