KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 13, 2018

MBOWE NA WENZAKE WASOMEWA MASHITAKA MAPYA

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na vigogo wengine saba wa chama hicho wamesomewa mashtaka mapya 13 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbowe na wenzake walisomewa mashtaka hayo jana  Juni 12 na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Hayo yamejiri baada ya upande wa mashtaka Juni 11, 2018 kuamriwa na mahakama wafanye marekebisho katika hati ya mashtaka baada ya kuonekana kuna ubatili na mapungufu ya kisheri.

Akisoma hati hiyo mpya iliyofanyiwa marekebisho katika kesi hiyo Namba 112 ya 2018 Nchimbi aliwasomea mashtaka washtakiwa nane kwa kuwa mwenzao Esther Matiko mbunge wa Tarime mjini hakuwepo mahakamani kwa kuwa ni mgonjwa.

Hivyo, Nchimbi aliwasomea mashtaka Mbowe, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba John Mnyika.

Wengine ni Katibu wa chama hicho Dk  Vicenti  Mashinji, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Baadhi ya mashtaka waliyosomewa ni kula njama na kufanya mkusanyiko usio halali, wenye ghasi na kukiuka tamko la kutawanyika, kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo, Februai 16 mwaka huu, barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni.

Mahakama ilielezwa kuwa, mkusanyoko huo ulipeĺekea hofu na hatimaye kifo cha Akwilina Akwilini, mwanafuni wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Usafirishaji(NIT)
Hakimu alisema mahakama itasikiliza maelezo ya awali Julai 18, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment