Shirika
la Maendeleo ya Petroli nchini TPDC, kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake
Mhandisi Kapuulya Musomba, limesaini mkataba wa miaka 20 wa kukipatia
kiwanda cha saruji cha Dangote, gesi asilia kama nishati kwa ajili ya
kuzalisha saruji.
Kufuatia
makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dar es salaam jana, kiwanda cha
Dangote kitaacha matumizi ya nishati ya mafuta katika uzalishaji na
kwamba mchakato wa kuhama kutoka matumizi ya mafuta kwenda ya gesi
utachukua kati ya siku 30 hadi siku 45 kuanzia sasa.
Hivi
karibuni kumekuwa na uhaba wa saruji katika soko ambapo kwa mujibu wa
Waziri wa Viwanda Mh. Charles Mwijage, moja ya sababu ni kupungua kwa
uzalishaji wa kiwanda cha Dangote hivyo kusainiwa kwa makubaliano hayo
kutasaidia kupunguza kuadimika kwa bidhaa ya saruji katika siku za usoni
ikiwa ni pamoja na bei kushuka.
Mradi
wa gesi asilia na iliyosindikwa Tanzania (TGP) ni miongoni mwa miradi
mikubwa zaidi ya ujenzi wa miundombinu katika historia ya Tanzania.
Matumizi ya gesi iliyopo nchini yataongeza uwezo wa nchi wa kusafirisha nje rasilimali hiyo na kuboresha miundombinu ya ndani.
Matumizi ya gesi iliyopo nchini yataongeza uwezo wa nchi wa kusafirisha nje rasilimali hiyo na kuboresha miundombinu ya ndani.
No comments:
Post a Comment