Vijana
30,000 kutoka Mikoa ya Iringa, Mbeya na Mikoa ya Tanzania Visiwani
watanufaika na fursa ya mafunzo ya kilimo na ujasiriamali kupitia
Program ya Feed the Future inayofadhiliwa na Shirila la Misaada la
Marekani (USAID) ambapo watapewa nyenzo na mtaji yenye thamani ya Sh.
Bilioni 11.
Hayo
yasememwa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana
na Ajira, Anthony Mavunde akiwa mkoani Iringa wakati akizindua Baraza
la Vijana la Ushauri wa Mradi.
Mavunde
alisema katika mradi huo vijana watapewa nyenzo na mitaji ya kuanzia
shughuli za uzalishaji mali, ambapo amelitaka Baraza hilo kuhakikisha
malengo ya mradi yanafikiwa hasa katika kumkomboa kijana wa kitanzania
na changamoto za ukosefu wa ajira na kumsaidia kufikia malengo yake.
Naye
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk.Inmi Patterson alisema Marekani
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza ujuzi wa Nguvu kazi ya
Vijana wa Tanzania na kuhamasisha ushiriki wao katika sekta ya kilimo
ili kuongeza pato la Taifa zaidi kupitia sekta ya Kilimo ambayo imeajiri
Watanzania wengi.
Kwa
upande wa Kaimu Mkuu Mkoa wa Iringa, Richard Kasesela ameahidi kutoa
ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo ambao utawanufaisha
Vijana wa Iringa kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment