Na Magdalena Kashindye
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amesema hana mpango wa kuhamia Chama cha mapinduzi CCM kwa sasa.
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amesema hana mpango wa kuhamia Chama cha mapinduzi CCM kwa sasa.
Kubenea
amekuwa akihusishwa kikihama chama chake cha CHADEMA tangu mwaka
jana, wimbi la viongozi, wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu
nafasi zao na kujiunga na kujiunga na CCM.
Juzi
aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akitetea
uamuzi wa viongozi wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM.
Ujumbe
huo wa mbunge Saed ulisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na
kuibua mjadala kutokana na kuhusishwa kwake kwa muda mrefu kujiunga na
chama tawala.
"Si
wote wanaohama wamenunuliwa, ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya
waliohama wamenunuliwa. Kuna wengine wamehama kutokana na kuwapo
migogoro, chuki na ubaguzi katika maeneo waliyokuwapo." ilisomeka hivyo posti ya Kubenea
Alipotafutwa
na Gazeti la Nipashe, kutaka kujua juu ya ujumbe wake alioposti
Kubenea alikiri kuuandika na kueleza kuwa kuhamia CCM kwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius
Mtatiro, kulimsukuma kuandika ujumbe huo.
"Ujumbe
huo ni kweli ni wa kwangu," Kubenea alisema, "niliandika baada ya
Julius Mtatiro kutangaza kuhama CUF na kujiunga na CCM.
"Inawezekana
hakunuliwa, lakini inawezekana njaa ndiyo imempeleka huko kwa sababu
kwanza ukumbuke chama chake kina mgogoro mkubwa, pia upande aliokuwa
yeye, hakuna ruzuku. Kwa hiyo, hawakuwa na pesa ya kujiendesha na ndiyo
maana akaona ahame tu.
"Nasema
hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao mimi nawafahamu, walihama na
hawakununuliwa isipokuwa walishindwa kuvumilia baada ya kukutana na
watu ambao walitofautiana nao kimawazo, yaani mawazo yao yalikinzana,
wao badala ya kuvumilia walishindwa."
Alipoulizwa
kuhamia CCM kama naye ni miongoni mwa wanaodaiwa wako kwenye njiani
kujiunga na CCM, Kubenea alisema hana mpango wa kukihama chama chake kwa
sasa.
Hii
ni mara ya pili kwa Kubenea kukana taarifa za kukihana chama chake
kwani wiki chache zilizopita alisema hawezi kahama na kama kunamapungufu
watayarekebisha ndani na akishindwa ataendelea na shughuli zake za
uandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment