Na Emanuel Madafa,Mbeya
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu
(3,000,000), Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Jamsi Sangu iliyopo Vwawa Mbozi Mkoani mbeya , ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake kufariki dunia ambaye alikuwa Said mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao .
Akizungumza katika makabidhiano hayo wilayani
Mbozi mkoani mbeya , Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, amesema mzazi wa mwanafnzi huyo Jaqline Ndyamkama ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha mtoto wake.
Amesema fao hilo la
elimu limekuwa msaada mkubwa kwa wategemezi mara baada ya wazazi kufariki dunia kwani imechangia kwa kiwango kikubwa wategemezi hao kukamilisha ndoto zao kwa uhakika zaidio licha ya kufiwa na wqzazi wao.
“Naomba Watanzania wote waweke utaratibu wa
kujiunga na bima hii ambayo malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver yakiwa ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.
Naye Jaqline
ameishukuru taaasisi hiyo ya Bayport kwa huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya mama yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kukamilisha ndoto zake kwani bado anasafari ndefu katika kufikia malengo ya kielimu huku pia akiwataka wazazi na walezi kujiunga na utaratibu huo.
Aidha kwa upande wake
bibi mlezi wa Jaqline Ndyamkama ,Angelika Geka , amesema hajawahi kuona taasisi yenye huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya kuhakikishiwa malipo ya mafao hayo ambayo tayari yamekwisha fanyika malipo ya ada ya mjukuu wake bila usumbufu wowote, jambo ambalo ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.
Aidha, utaratibu wa
malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao umepangwa kulipwa kila mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo yananufaisha walengwa, hususan kwa wale wanaoendelea na masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini. |
July 21, 2015
TAASISI YA KIFEDHA YA BAYPORT YAKABIDHI HUNDI YA MIL 3 KWA WATEGEMEZI WA FAO LA ELIMU MKOANI MBEYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment