Add captionKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH) |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa hospitali hiyo. |
Wajumbe wakipiga kura LEO za kuwachagua viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hiyo. |
Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo. |
Wakili Eneza Msuya akiwashukuru LEO wajumbe baada ya kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo. |
Kutoka kushoto ni Katibu wa
Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa Mwambene, Mwenyekiti
wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa
Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo, Wakili Eneza Msuya na
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.
………………………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya
ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya
watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.
Akizindua Baraza la Wafanyakazi
la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua
hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa
bidii.
“Nimefarijika sana kuoana
suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli
mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu,
lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na
maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
Akizungumza kabla ya uzinduzi
wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo
imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea
kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto
wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa
maisha ya mama na mtoto .
Kwa mujibu wa Profesa Museru
Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma
za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza
la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza
hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
|
No comments:
Post a Comment